Uhuru adai Mashirika ya Kijamii yanatumiwa kutatiza uchaguzi mkuu 2017 

Mashirika ya kijamii yanayopata ufadhili kutoka mataifa ya ughaibuni yanatarajiwa kujibu madai ya Rais Uhuru Kenyatta kuwa yanafadhiliwa ili kuwahamasisha wananchi kuhusu masuala ya upigaji kura.

Kwa mujibu wa Uhuru, mataifa hayo yanayotoa ufadhili yanalenga kutatiza uchaguzi mkuu ujao huku akiongezea kuwa atakubali kushindwa iwapo wapiga kura wataamua kuibandua serikali ya Jubilee.

Akihutubu wakati wa maadhimisho ya hamsini na mbili ya siku ya Jamhuri, Uhuru amewashauri wananchi kutoshawishika na mashirika hayo na badala yake kufanya uamuzi wao wenyewe wakati wa kupiga kura.

Hii si mara ya kwanza kwa serikali kutoa madai haya, katikati ya mwaka huu, Msemaji wa serikali Eric Kiraithe alidai kuwa baadhi ya wanasiasa wanatafuta ufadhili kutoka ng’ambo ili kulemaza utawala wa Jubilee.

http://www.standardmedia.co.ke/?articleID=2000226659 via @StandardKenya

Advertisements