Asiyejua kufa naye atazame kaburi.
Nilimthamini hadi nikafahamu mtimani ya kuwa mapenzi ni kipenzi na sabuni ya roho.
Pasi na kufahamu mapenzi ni kati ya watu wawili au zaidi! Huu ndio wak’ti ilibidi mwana wa msomi nilazimike kuelewa.
Siku baada ya nyengine moyo ulianza kutamani kupendwa,ingawa bado nlikuwa sijamakinika na swala hili zima la mahaba.
Na kama kweli wasemavyo wavyele,

asiyejua maana haambiwi

maana.

Tangu

image

nlipokupata weye kamusi nikaipata……kwani aliye na kamusi hatatizwi na neno!
Lakini ka kuahangaza hili hapa,tutafakarini sote…. Mapenzi bila pesa ni kama baiskeli bila pumzi,kanieleza Kalameni.
Nafikia kuliamini hilo baadae kwa maana kaniona mie benki! “Kaka ninulie vibanzi” basi hapo tumeelewana twanyoosha miguu mtaani-Haya basi nkanunua,si wangu mpenzi huyi.
Dah! Darling, wanavoita hao..”nywele nazo si nishukwe” kaniona na sarafu huyu,pia nataka ajue mie nshikaji wake kweli,nikampeleka kwa shangazi yangu anshuke…”mimi uko siendi,sijutaki huko.” Balaa kaingia.
Su kwa msusi uko…..(

itaendelezwa)

Nariari Auliver™
©2015

Advertisements